Chombo cha China cha kufanya utafiti kwenye bahari ya kina kirefu chakamilisha kazi kwenye Babari ya Kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2025
Chombo cha China cha kufanya utafiti kwenye bahari ya kina kirefu chakamilisha kazi kwenye Babari ya Kusini mwa China
Chombo kilichoundwa na China kwa kujitegemea cha Haiqin, kinachoweza kuendeshwa kwa udhibiti kutoka mbali (ROV) kwenye kina kirefu cha mita 6000 baharini, kimetolewa baharini, na kinawekwa kwenye meli ya Zhong Shan Da Xue, katika Bahari ya Kusini mwa China, Agosti 23, 2025. (Xinhua/Zhang Jiansong)

Chombo kilichoundwa na China kwa kujitegemea kinachoweza kuendeshwa kwa udhibiti kutoka mbali (ROV) kwenye kina kirefu cha mita 6000 baharini, kimetolewa kutoka baharini, baada ya kukamilisha kwa mafanikio safari ya kina kirefu katika Bahari ya Kusini mwa China.

Kwenye majaribio ya baharini yaliyofanyika mapema Jumamosi asubuhi, Chombo hicho cha Haiqin, kilichosanifiwa na kuundwa na Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Shanghai kimeweza kufika kina cha mita 4,140.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha