Idadi ya kulungu pori wa Milu yaongezeka tena nchini China baada ya juhudi za miaka 40 ya uhifadhi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 26, 2025
Idadi ya kulungu pori wa Milu yaongezeka tena nchini China baada ya juhudi za miaka 40 ya uhifadhi
Watafiti wa Kituo cha Kitaifa cha Hifadhi na Utafiti cha Milu wanakusanya sampuli katika Bustani ya Milu mjini Beijing, China, Agosti 18, 2025. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Shughuli mbalimbali zilifanyika Jumapili kwenye Hifadhi ya Milu kusherehekea miaka 40 tangu kurejeshwa kwa kulungu aina ya milu nchini China. Kulungu aina ya Milu, ambaye pia anajulikana kuwa ni kulungu wa Pere David, ni wa kulungu wa kawaida nchini China ambao wana jina la utani "sibuxiang", neno ambalo maana yake ni "asiyefanana na wale wanne" kutokana na sifa zao za kipekee, uso wa kifarasi, mkia wa kipunda, kwato zinazofanana na ng'ombe na pembe za kulungu.

Kulungu mwitu wa milu walitoweka nchini China na kuletwa kutoka ng'ambo mwaka 1985. Aina ya wanyama hao sasa iko chini ya ulinzi wa ngazi ya kwanza nchini China. Baada ya miaka 40 ya juhudi zisizo na ukomo, China sasa imejengea upya kundi la wanyama hao wa pori na kushuhudia idadi ya kulungu wa Milu wanaozaliwa kwa njia isiyo ya jadi ikiongezeka.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha