

Lugha Nyingine
Rais wa Botswana atahadharishwa kuhusu tishio la dawa mseto zinazofanywa kazi kama mihadarati (2)
![]() |
Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya, Masuala ya Kibinadamu, na Maendeleo ya Jamii, Bibi Amma Twum-Amoah akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Dunia la Umoja wa Afrika kuhusu Kupunguza Upatikanaji wa Dawa mseto zinazofanana na mihadarati huko Gaborone, Botswana, Agosti 25, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo) |
GABORONE -- Rais Duma Boko wa Botswana ametoa wito wa kuimarishwa kwa umoja wenye nguvu na unaoendeshwa kwa kutumia taarifa za kijasusi kati ya nchi za Afrika, ili kukabiliana na msukosuko unaoongezeka wa dawa mseto zinazofanana na mihadarati.
Akizungumza mjini Gaborone kwenye ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Dunia la Umoja wa Afrika (AU) kuhusu kupunguza upatikanaji wa dawa mseto zinazofanana na mihadarati, Rais Boko amezungumzia changamoto ya hali ya kuvuka nchi ya dawa hizo, kuwa ni tishio lililo nje ya utekelezaji wa sheria za kawaida.
Ameeleza kwa kina jinsi makundi ya wahalifu yanavyotumia teknolojia ya kisasa kusafirisha dawa haramu na kupata faida kwa kutumia njia zenye utatanishi, na kuhatarisha usalama wa kikanda na afya ya umma. Rais Boko amesema, jibu ni lazima liwe la haraka na la kimkakati, akisisitiza kuwa ni lazima liwe na msingi kwa polisi wanaoongozwa na taarifa za kijasusi, kuimarishwa kwa ushirikiano wa kikanda, mifumo ya kisheria, na ushiriki wa makini wa jamii, na kuongeza kuwa mitandao ya wahalifu isiachwe ifanye kazi bila kuadhibiwa.
Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Afya, Masuala ya Kibinadamu, na Maendeleo ya Jamii, Bibi Amma Twum-Amoah, alieleza mkakati wa Umoja wa Afrika wenye pande nyingi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mifumo ya tahadhari ya mapema ya bara la Afrika, kuweka majukwaa jumuishi ya data, na kuimarisha ujenzi wa uwezo wa nchi wanachama.
Mkutano huo wa siku tatu unafanyika chini ya kaulimbiu, "Kuimarisha Juhudi za kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya na Kuimarisha kuzuia uhalifu, Kutekeleza haki, na Utawala wa Sheria Barani Afrika."
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma