Watu wa kabila la Wamiao washerehekea Mwaka Mpya wao wa jadi katika Mkoa wa Guangxi, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2026
Watu wa kabila la Wamiao washerehekea Mwaka Mpya wao wa jadi katika Mkoa wa Guangxi, China
Wanakijiji wakishiriki kwenye sherehe za Mwaka Mpya wa jadi wa kabila la Wamiao katika Kijiji cha Dangjiu cha mji Gandong wa Wilaya inayojiendesha ya kabila la Wamiao ya Rongshui, Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Januari 20, 2026. (Xinhua/Huang Xiaobang)

Watu wa kabila la Wamiao katika Kijiji cha Dangjiu cha Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, wamesherehekea Mwaka Mpya wa jadi wa kabila la Wamiao jana Jumanne, Januari 20. Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa Wamiao pia inajulikana ni siku ya kipindi cha Dahan, yaani Baridi Kubwa kwenye kalenda ya kilimo ya China, ni sikukuu kubwa ya watu wa kabila la Wamiao. Mwaka 2008, sikukuu hiyo iliorodheshwa kuwa mali ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha