Lugha Nyingine
Shughuli ya "ladha za kijijini" yafanyika katika Wilaya ya Shiqian, Guizhou, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2026
![]() |
| Watu wakishiriki kwenye shughuli ya kuonesha "ladha za kijijini" katika Wilaya ya Shiqian ya Mji wa Tongren, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Juni 27, 2026. (Picha na Sun Wei/Xinhua) |
Katika siku ya mwishoni mwa wiki iliyopita, shughuli ya kuonesha "ladha za kijijini" imefanyika katika Wilaya ya Shiqian ya Mji wa Tongren, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China. Timu kutoka vijiji au maeneo ya wakazi zaidi ya 10 zimeshiriki katika mashindano ya kupika vyakula kwa kutumia viungo vya kienyeji kama vile chai ya moss ya Shiqian na mazao ya kilimo ya majira ya hivi sasa. Watu walifanya maadamano ya kuonesha mali za urithi wa utamaduni usioshikika, kufanya mashindano ya burudani na shughuli nyingine kwa kuonyesha vyakula vya sehemu zao na mila na desturi za kijijini.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




