Lugha Nyingine
Kampuni za Wilaya ya Cheng'an mkoani Hebei zakumbatia uchumi wa kidijitali kwa kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2026
![]() |
Wilaya ya Cheng'an ya Mji wa Handan katika Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China imekumbatia uchumi wa kidijitali na kubadili viwanda vyake kuwa injini ya kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora.
Wilaya hiyo imeanzisha timu mahsusi ya kutangaza moja kwa moja mtandaoni mazao ya kilimo au bidhaa yenye sifa bora ya wilaya hiyo ili kuondoa vizuizi vya kawaida kati ya wazalishaji na wanunuzi, na kuhimiza kampuni na viwanda vya wilaya hiyo kuunganisha matangazo ya mtandaoni na nje ya mtandaoni. Mwaka 2026, thamani ya jumla ya uuzaji wa mazao ya kilimo au bidhaa wa kampuni na viwanda vilivyoshiriki katika mpango huo imefikia yuan milioni 110 (dola za Marekani takribani milioni 16.18).
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




