Tarehe 22, Septemba, vipeperushi vya matangazo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 vilitolewa kwenye hafla ya ufunguzi wa Wiki ya ubunifu ya kimataifa ya Beijing.
“Twendeni pamoja siku za baadaye”! “Together for a Shared Future”! Septemba, 17, Beijing, Jumba la Makumbusho la Mji Mkuu. Wakati wa siku zinazobaki 140 kabla ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya baridi ya Beijing, wito wa michezo hiyo ya Olimpiki ya mwaka 2022 umetolewa.
Tarehe 16, Agosti, shughuli za “Kujiunga na Kunufaika” za kumbukumbu ya Siku 200 zinazobaki kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya majira ya baridi ya Beijing zilifanyika kwenye eneo la ofisi za Shougang za Tume ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing, shughuli hizo zilionesha matokea ya kazi ya mafunzo kwa umma kuhusu Michezo ya Olimpiki ya walemavu hasa mafunzo hayo kwa vijana na watoto.
Michezo ya 32 ya Olimpiki ya majira ya joto imefungwa, wakati wa Michezo ya Olimpili umeingia ratiba ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing. Tarehe 9, Septemba, kampuni inayomilikiwa kitaifa ya Beijing, ambayo ni kampuni inayobeba jukumu la kujenga na kukarabati majengpo matatu ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya “Kiota cha Ndege”, “Mchemraba wa Maji” na “Ukanda wa Barafu”, inaeleza kwamba, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya majira ya baridi ya Beijing 2022, sherehe ya kufunguliwa na kufungwa kwa michezo zitafanyika kwenye Uwanja wa Kitaifa wa China (Kiota cha Ndege), hivi sasa Kiota cha Ndege kimeingia katika kipindi cha ujenzi na ukarabati, ambao utakamilika Oktoba, mwaka huu kwa mpango uliowekwa.