人民网首页

Habari

“Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inaonesha uthabiti wa michezo katikati ya janga la UVIKO”

DUBAI – Vyombo mbalimbali vya habari vya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu vimeripoti kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inayoendelea mjini Beijing, nchini China imethibitisha kwa Dunia utahimilivu wa michezo katikati ya janga la UVIKO-19. Licha ya changamoto kubwa chini ya hali ya sasa, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing imepata "mwanzo mzuri pamoja na hatua zote zilizowekwa ili kuhakikisha usalama wa wale wanaoshiriki," inasema tahariri ya Gulf News, gazeti la kila siku la Kiingereza huko Dubai.

Mathilde Greymode (katikati) kutoka Uswizi aliyenyakua ubingwa, Gu Ailing (kushoto) wa Timu ya China aliyepata nafasi ya pili, na Kelly Hildalu wa Estonia aliyepata nafasi ya tatu wakiwa kwenye hafla ya kutunukiwa zawadi ya kumbukumbu Februari 15. (Picha/Xinhua)

Gu Ailing Ashinda Medali ya Fedha Kwenye Mchezo wa kuteleza kwenye barafu katika mteremko mkali na kuruka hewani

Siku hiyo, mchezaji wa Timu ya China Gu Ailing amepata nafasi ya pili katika fainali ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu katika mteremko mkali na kuruka hewani kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, mchezo ambao ulifanyika kwenye Bustani ya Yunding ya kuteleza na kuruka hewani kwenye theluji ya Zhangjiakou, China.

Eneo la Kitanzi la kudhibiti UVIKO-19 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni thabiti: The Independent

Wanamichezo wakishiriki katika mazoezi kabla ya raundi ya 8 ya mchezo wa Curling kwa Wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kati ya Japani na Korea Kusini katika Kituo cha Taifa cha Kuogelea huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 14, 2022. (Xinhua/Huang Xiaobang) LONDON, Februari 14 (Xinhua) – Gazeti la Uingereza la The Independent limesema kwamba, kuleta zaidi ya watu 15,000 kutoka pembe zote za Dunia hadi Beijing kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kunaleta hatari kubwa ya kuenea UVIKO-19 nchini China.

Timu ya China yaweka rekodi bora linganifu kwa medali za dhahabu ilizopata kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

Xu Mengtao mwenye umri wa miaka 31 ambaye ameshiriki kwa mara nne kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi hatimaye ametimiza ndoto yake hapa Beijing. Ametwaa medali ya dhahabu kwa mchezo wa kuteleza kwa ustadi kwa mtindo huru kwenye theluji kwa wanawake.

Iliyopita5 6 7 8 9 10 Inayofuata