Kwenye sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing, mshika bendera wa Samoa ya Marekani Nathan Crumpton hakuhofia baridi na alionekana katika mwili wake uliotiwa mafuta bila kuvaa shati, alivaa sketi ya nyasi na makubadhi. Baada ya sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo, alipewa jina la "mshika bendera aliyeganda zaidi kwa baridi katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi" na watazamaji wa China na wa kigeni.
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwenye hafla ya kuwakaribisha wageni mashuhuri kutoka duniani kote waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 5, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ameshiriki katika mikutano ya ana kwa ana ya ngazi ya juu na viongozi wa kigeni waliofanya ziara mjini Beijing kwa ajili ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing licha ya changamoto zinazosababishwa na janga la UVIKO-19.
Siku hiyo mchezaji wa Timu ya China Gu Ailing ametwaa ubingwa katika fainali ya mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kuruka angani kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, mchezo ambao ulifanyika kwenye Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang ya Beijing, Mji Mkuu wa China. (Xinhua/ Mpiga picha: Xue Yuge).
Fainali ya mchezo wa kuteleza kwa ubao kwenye theluji katika mteremko katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 ilifanyika Februari 7 kwenye Ukumbi ulioko kwenye Bustani ya kuteleza kwenye theluji ya Yunding, Zhangjiakou. Mchezaji wa Timu ya China Su Yiming alishinda medali ya fedha katika mchezo huo.