Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Zimbabwe Amon Murwira (kulia) na Naibu Waziri wa Biashara wa China Zhang Li wakipiga picha ya pamoja, Harare, Zimbabwe, Agosti 26, 2026. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua) HARARE - China na Zimbabwe zimesisitiza azma zao katika kuzidisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili kwenye Mkutano wa 11 wa Kamisheni ya Pamoja juu ya Ushirikiano wa Kiuchumi, Kiufundi na Biashara katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
BEIJING - Wizara ya mambo ya nje ya China imetangaza jana Jumatano kwamba kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 3, Rais wa China Xi Jinping atahudhuria Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) 2026 mjini Bishkek, na kufanya ziara ya kiserikali nchini Kyrgyzstan na Misri kutokana na mwaliko wa Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan na Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa habari zaidi kuhusu safari hiyo, msemaji wa wizara hiyo Lin Jian amesema, mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa SCO.
Waziri wa Elimu ya Juu wa Botswana, Prince Maele, akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano, huko Gaborone, Botswana, Agosti 24, 2026. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua) GABORONE - Wizara ya Elimu ya Juu ya Botswana na kampuni ya uchimbaji wa Shaba ya Khoemacau inayowekezwa na China jana Jumatatu wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuanzisha Kituo cha Ubora cha Uchimbaji wa Madini kwenye Chuo cha Ufundi cha Maun katika sehemu ya Kaskazini Magharibi ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ili kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa wafanyakazi wa kiufundi wa sekta ya madini ya nchi hiyo.
Jukwaa la 7 la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika lenye kaulimbiu ya "Kunufaika Pamoja na Fursa za Maendeleo, Kujenga Siku za Baadaye za Utangazaji wa TV na Radio" limekuwa likifanyika Beijing, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Julai 19 hadi 21.