人民网首页

Habari

Kampuni za China na Ethiopia zasaini mikataba yenye thamani ya dola milioni 330 za Marekani kwenye shughuli ya kutangaza biashara

Chen Hai, balozi wa China nchini Ethiopia, akizungumza kwenye Mkutano wa Ethiopia wa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" mjini Addis Ababa, Ethiopia, Agosti 19, 2026. (Xinhua/Geng Xinning) ADDIS ABABA - China imezindua Mkutano nchini Ethiopia unaoitwa "Soko Kubwa kwa Wote: Mauzo ya Nje kwa China" Jumatano wiki hii mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha na kupanua mauzo ya nje ya bidhaa za Ethiopia kwenye soko la China.

Ushirikiano wa huduma ya afya wa China-Tanzania waleta utambuzi magonjwa kwa kutumia AI kwa wagonjwa

Picha hii iliyopigwa Mei 28, 2026 ikionyesha Yuan Gang, mtaalamu wa mionzi katika kundi la 35 la timu ya matibabu ya China visiwani Zanzibar, akijadili picha za MRI na madaktari wenyeji kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, Tanzania. (kundi la 35 la timu ya matibabu ya China visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua) DAR ES SALAAM – Ndani ya chumba cha mionzi katika Hospitali ya Mkoa ya Lumumba visiwani Zanzibar, Tanzania mabadiliko ya kimyakimya ya teknolojia yanabadilisha namna madaktari wanavyobaini magonjwa, kufanya maamuzi, na kuokoa maisha.

China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika katika kupambana na Ebola

BEIJING - Lin Jian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema kwamba, kwa kuwa mlipuko wa Ebola bado unaenea barani Afrika, China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika na kutoa uungaji mkono unaohitajika ili mlipuko huo uweze kukomeshwa mapema iwezekanavyo. Lin ameyasema hayo jana Jumanne alipokuwa akijibu swali kuhusu timu ya tatu ya wataalamu wa matibabu iliyotumwa na serikali ya China iliyofika Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Agosti 1.

Kampuni ya China yazindua mpango wa kukuza vipaji kuchochea maendeleo ya miundombinu ya Cameroon

Wageni wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya mafunzo baada ya hafla ya uzinduzi, Yaounde, Cameroon, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Kepseu) YAOUNDE – Kampuni ya Uhandisi ya First Highway ya China (CFHEC) imezindua mpango wa mafunzo uliopewa jina la Mpango wa Vipaji wa Seagull jana Jumatatu ili kujenga utaalamu wa wenyeji nchini Cameroon.

Iliyopita2 3 4 5 6 7 Inayofuata