Sikukuu ya Mashua ya Dragoni yasherehekewa kote China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2025
Sikukuu ya Mashua ya Dragoni yasherehekewa kote China
Watoto wakijaribu kutengeneza zongzi kwa mikono yao, chakula cha kijadi cha China kuadhimisha Sikukuu ya Mashua ya Dragoni, katika kituo cha elimu ya mazingira ya asili katika Mji mdogo wa Xiaochang wa Mji wa Zunhua, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, Mei 30, 2025. (Picha na Liu Mancang/Xinhua)

Sikukuu ya Mashua ya Dragoni, ambayo pia inajulikana kwa jina la Sikukuu ya Duanwu kwa Kichina, ni sikukuu ya jadi ya China kumkumbuka mshairi wa China ya kale Qu Yuan kutoka Enzi ya madola ya kivita (475-221). Ikiwa inasherehekewa siku ya tano ya mwezi wa tano kwa kalenda ya kilimo ya China, sikukuu hiyo, kwa mwaka huu iliangukia Mei 31 ambapo Wachina walikuwa na mapumziko ya siku tatu yaliyofikia tamamati jana Jumatatu. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha