人民网首页
Picha hii iliyopigwa Oktoba 14, 2023 ikionyesha mapambo ya maua kwa ajili ya Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirkiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) karibu na Kituo cha Mikutano cha Taifa cha China mjini Beijing, China. (Xinhua/Ju Huanzong)

Zaidi ya nusu ya miradi ya ushirikiano iliyofikiwa kwenye Mkutano wa BRF yaanza kutekelezwa

Picha hii iliyopigwa Oktoba 14, 2023 ikionyesha mapambo ya maua kwa ajili ya Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirkiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) karibu na Kituo cha Mikutano cha Taifa cha China mjini Beijing, China. (Xinhua/Ju Huanzong) BEIJING - Zaidi ya nusu ya jumla ya miradi 369 ya ushirikiano iliyofikiwa kwenye Mkutano wa 3 wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRF) imeanza kutekelezwa kwa sasa, kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC) iliyotolewa siku ya Alhamisi.…

Picha hii ya angani iliyopigwa Aprili 26, 2023 ikionyesha eneo la ujenzi wa Reli Kiunganishi ya Pwani ya Mashariki (ECRL), mradi mkubwa wa miundombinu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) mjini Kelantan, Malaysia. (Xinhua/Zhu Wei)

BRI yaleta muunganisho ulioimarishwa kwa maendeleo na ustawi wa pamoja: wataalam

KUALA LUMPUR – Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililotolewa na China limesonga mbele muongo mmoja tangu kuzinduliwa kwake na linaendelea kukua katika wigo na kiwango, na kuleta muunganisho bora wa miundombinu kwa maendeleo na ustawi wa pamoja, wataalam wamesema kwenye kongamano la kimataifa lililofanyika Kuala Lumpur, Malaysia. Kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Asia Mpya Jumuishi (IFNIA) 2023 siku ya Jumatatu, Ong Tee Keat, Mkuu wa Taasisi ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ya Asia Pasifiki ametoahotuba akisifu mafanikio madhubuti yaliyofikiwa na BRI katika muongo mmoja uliopita.…

Wasafiri wanaoelekea ng'ambo wakipanda basi la abiria kwenye Kivuko cha Khunjerab katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Watajik la Taxkorgan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Ding Lei)

Kivuko cha Khunjerab, bandari kuu ya nchi kavu inayounganisha China na Pakistan

Kikiwa kinapatikana katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Watajik la Taxkorgan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Kivuko cha Khunjerab ni bandari kuu ya nchi kavu kwenye mpaka wa China na Pakistani, kituo kikuu cha biashara kati ya China na Pakistani, na lango muhimu la kuingia Asia Kusini na Ulaya. Tangu kuanza upya kwa utoaji vibali vya forodha kwa abiria Mwezi Aprili 3, 2023, Kivuko cha Khunjerab kimerekodi abiria zaidi ya 40,000 wanaoingia na kutoka.…