Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limepita miaka kumi: Barabara zimeunganishwa na uzuri umechangiwa na Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 28, 2023

Katika majira ya mpukutiko ya Mwaka 2013, Rais Xi Jinping wa China alitoa mapendekezo makuu ya kujenga kwa pamoja "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri" na "Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21". Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, China na nchi zinazotekeleza kwa pamoja mapendekezo hayo mawili, zimekuwa zikisonga mbele bega kwa bega, na miundombinu ikiwa ni moja ya mwelekeo muhimu. Katika "msafara wa ngamia wa chuma" usio na mwisho, kwenye daraja lenye shughuli nyingi la kuvuka bahari, na katika mwinuko wa mita 10,000 kwenye "Njia ya Hariri ya Angani"... ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umebadilishwa kutoka dhana hadi vitendo. Katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kutolewa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", tovuti hii inaangazia mafanikio makubwa na ya dhahiri yaliyopatikana katika ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kutoka mtazamo wa pande tatu za muunganisho wa miundombinu ya ardhini, baharini na angani.

Juu ya ardhi – dragoni mkubwa wa chuma anakimbia bila kikomo

蒙内铁路

• Reli ya Kenya ya Mombasa-Nairobi

Mnamo Mei 31, 2017, reli hiyo ilikamilishwa na kufunguliwa rasmi kwa matumizi ya umma.

Reli hiyo ya kwanza kujengwa nchini Kenya tangu nchi hiyo ipate uhuru, ni reli ya kisasa iliyojengwa kwa vigezo vya China, teknolojia ya China na vifaa vya China.

Ujenzi wa reli hio ulitoa nafasi za ajira zaidi ya 74,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja nchini Kenya, kuwaandaa vipaji zaidi ya 2,800 vya ufundi na usimamizi wa reli, na kuongeza Pato la Taifa la Kenya kwa angalau 2%.

Hadi kufikia Septemba 30, 2023, Reli ya Mombasa-Nairobi imesafirisha makontena jumla ya milioni 2.405 ya kawaida na kusafirisha mizigo kwa tani milioni 28.609. Abiria jumla ya milioni 11.155 wamesafirishwa, wakiwa ni wastani wa ujazaji vya viti wa 95.8% kwenye treni, na idadi kubwa zaidi ya abiria waliosafiri kwa siku moja ilizidi 10,000.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha