人民网首页

Rais Xi Jinping ahimiza China na Afrika kuungana mkono kwa ajili ya maendeleo ya kisasa

BRICS yatangaza nchi wanachama wapya sita

Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa mfumo wa ushirikiano wa nchi za BRICS unaofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini umeamua kuzikaribisha nchi za Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa wanachama wapya.

Nchi wanachama wa BRICS zakubali kuzidisha ushirikiano ili kuhimiza uimarikaji endelevu wa utalii

Nchi wanachama wa BRICS ambazo ni pamoja na Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zimekubaliana kuzidisha ushirikiano ili kufikia uimarikaji endelevu na jumuishi kwenye sekta ya utalii. Nchi hizo zimeeleza hayo katika taarifa ya pamoja iliyosainiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa utalii wa nchi za BRICS iliyotolewa siku ya Jumanne mjini Cape Town.…

Mtaalam asema Ushirikiano wa dhati kati ya Afrika na China unaleta manufaa yanayoonekana na maendeleo kwa pamoja

LUANDA - Ushirikiano wa dhati wa China na nchi za Afrika unazaa "matunda yanayoonekana na ya kuhimiza juhudi" ambayo yanaleta manufaa ya pande zote na maendeleo kwa pamoja, amesema mtaalam wa Angola. Kwenye ushirikiano kati yake na Afrika, China imeweka msingi muhimu wa miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika bara zima, na hivyo kuleta ukuaji wa viwanda na kuongeza thamani ya kibiashara ya bara la Afrika, amesema Osvaldo Mboco, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Angola katika mahojiano yake kwa njia ya maandishi na Shirika la Habari la China, Xinhua kufuatia Mazungumzo ya Viongozi Wakuu wa China na Afrika yaliyofanyika Alhamisi nchini Afrika Kusini.…

Mtaalam wa Ethiopia asema hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS itasaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Huduma za Jamii nchini Ethiopia Mukerrim Miftah amesema, hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS inatarajiwa kuchochea kidhahiri ukuaji wa uchumi na kuimarisha manufaa yake ya kunufaishana ya kikanda. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Miftah amesema hatua hii ni ya msingi kwa sababu kadhaa, ikiwemo kuisaidia Ethiopia kujenga ushirikiano wa nguvu wa kiuchumi na kisiasa na nchi wanachama wa BRICS, kusaidia uhusiano mzuri wa uchumi, biashara na uwekezaji kati yake na nchi mpya na zile zilizopo katika kundi la BRICS.…

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi.(Picha na mhojiwa)

Msomi wa Tanzania: nchi za Afrika zatakiwa kuhamasishwa kujiunga na mfumo wa BRICS

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi.(Picha na mhojiwa) Mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti huko Johannesburg, Afrika Kusini, kaulimbiu ya mkutano huo ni “BRICS na Afrika: kuimarisha uhusiano wa wenzi, kuhimiza ongezeko kwa kila upande, kutimiza maendeleo endelevu, kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi wa kijumuishi”.…