人民网首页

Timu ya madaktari Wachina yaleta huduma ya afya bila malipo kwa jamii ya Zanzibar, Tanzania

Asubuhi ya Jumamosi yenye mwanga angavu huko Kombeni, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar, Tanzania, mfanyakazi wa ulinzi mwenye umri wa miaka 71 Amin Maulid Juma alitoka kwenye Kliniki ya Sinai akiwa na hisia mpya ya unafuu na shukrani. Kwa wiki kadhaa, alikuwa amevumilia usiku mfululizo wa kukosa usingizi kutokana na maumivu ya tumbo yasiyokoma. Lakini baada ya dakika 45 tu chini ya uangalizi wa madaktari kutoka kundi la 35 la timu ya madaktari ya China visiwani Zanzibar, hali yake iliboreka sana.

Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China,inayoitwa “Meli ya Baraka” inatia nanga katika Bandari ya Urafiki huko Nouakchott, Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Meli ya hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Mauritania kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu.

Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China, inayoitwa "Meli ya Baraka" inatia nanga katika Bandari ya Urafiki huko Nouakchott, Mauritania, tarehe 15 Septemba 2026. (Xinhua/Xie Jianfei) Meli ya hospitali ya Jeshi la Majini la China, inayoitwa "Meli ya Baraka (Auspicious Ark)" iliwasili Jumanne nchini Mauritania kwa ziara ya kirafiki ya siku saba, ambapo itatoa huduma za matibabu.…

China yaendelea kuwa nchi mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa EAC

China imeendelea kuwa nchi mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika robo ya pili (Q2) ya 2026, wakati thamani ya jumla ya biashara zake na eneo hilo ikikua kwa asilimia 37 ikilinganishwa na mwaka jana na kufikia dola bilioni 52.3.…

Afrika Kusini yatafuta ushirikiano wa kina zaidi na China katika sayansi na uvumbuzi

Katibu Mkuu wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi ya Afrika Kusini, Mlungisi Cele, amesema Afrika Kusini inatafuta ushirikiano wa kina zaidi na China kwenye sayansi, teknolojia na uvumbuzi, kufuatia ushiriki wake katika Kongamano la 19 la Uvumbuzi la Pujiang mjini Shanghai. Bw.…

Droni zikipangiliwa kuonesha tendo la kushikana mikono na Ukuta Mkuu wa China kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

Maonesho ya mwanga wa droni yaangaza mabadilishano kati ya watu wa China na Botswana

Droni zikipangiliwa kuonesha tendo la kushikana mikono na Ukuta Mkuu wa China kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo) GABORONE - Maonesho ya mwanga wa taa za droni 500 zilizopangiliwa kwa maumbo maaulum Jumanne usiku wiki hii yalivutia mamia ya watazamaji kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana, ili kuonesha urafiki na mabadilishano kati ya watu wa China na Botswana.…