Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (10)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

X. Kiwango cha matumizi ya kila siku ya barabara kuu ya Nairobi iliyojengwa na China chafikia magari 50,000

(Picha inatoka ChinaDaily.)

Barabara Kuu ya Nairobi iliyojengwa na China ambayo inaanzia upande wa Magharibi wa jiji hadi upande wa Kusini Mashariki mwa jiji hilo kwa sasa inarekodi wastani wa kila siku wa magari 50,000, mwendeshaji wa mradi huo amesema mwezi wa Disemba.

Barabara Kuu ya Nairobi imefadhiliwa na kujengwa na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC), na ilianza majaribio mwezi wa Mei mwaka huu. Mwaka 2022, miradi mingi ya miundombinu chini ya ushirikiano wa China na Afrika ilizinduliwa, kama vile daraja jipya la Mto Wami nchini Tanzania, kituo cha kuzalisha umeme cha Sakai, ambacho ni kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati; Mfumo wa kwanza wa reli ya kutumia umeme ya Misri (LRT) uliojengwa kwa pamoja na makampuni ya China na Misri; sehemu ya kwanza ya makao makuu ya kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Afrika......majengo hayo marefu na barabara hizo pana ni alama ya urafiki wa dhati kati ya China na nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha