

Lugha Nyingine
Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (2)
II. Ushirikiano wa chanjo kati ya China na Afrika wafanya kazi vizuri
Waziri wa Afya wa Zambia Sylvia Masebo (wa pili kutoka kushoto, mbele) na Balozi wa China nchini Zambia Li Jie (wa kwanza kulia, mbele) walihudhuria hafla ya kuwasili kwa chanjo dhidi ya UVIKO-19 zilizotolewa na China kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda mjini Lusaka, Zambia, Januari 24, 2022.
Ili kuzisaidia nchi za Afirka kupambana na maambukizi ya virusi vya korona, serikali ya China imezizawadia Zambia, Tanzania, Misri, Tunisia na nchi nyingine za Afrika chanjo dhidi ya UVIKO-19. Takwimu zinaonyesha kuwa, tangu kufanyika kwa mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) hadi mwezi wa Agosti mwaka huu, China imetoa dozi milioni 189 za chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa nchi 27 za Afrika, ikihimiza uzalishaji wa chanjo kwa kushirikiana barani Afrika ili ufikie dozi milioni 400.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (Afrika CDC) Ahmed Ogwell Ouma alisema, ushirikiano kati ya China na Misri, Algeria, na Morocco umeipa Afrika chanzo mbadala cha chanjo dhidi ya UVIKO-19, hasa katikati ya Mwaka 2021 ambapo hali ya maambukizi ilikuwa mbaya zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma