

Lugha Nyingine
Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (5)
V. Teknolojia ya Juncao ya China yaleta matumaini kwa wapandaji uyoga wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Picha hii iliyopigwa Tarehe 1, Juni, 2022, ikionesha mtaalamu wa China akipanda uyoga pamoja na wakazi wa Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Xinhua/Luo Yu)
Kuanzia mwezi wa Mei, 2021, wataalamu wa mradi wa teknolojia ya Juncao wa kusaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati waliwasili nchini humo. Kiongozi wa mradi huo Chen Kehua alisema, hadi Mwezi Julai mwaka huu, walikuwa wameandaa semina mara 16 kutoa mafunzo juu ya teknolojia ya Juncao, ambapo wanafunzi 613 walishiriki kwenye semina hizo
Teknolojia ya Juncao ilivumbuliwa na mwanasayansi wa China Lin Zhanxi, na imekuwa ni tasnia muhimu ya kuondoa umaskini nchini China. Mnamo Mwaka 2017, teknolojia hiyo kutoka China iliorodheshwa kuwa mradi muhimu wa uhimizaji wa Mfuko wa Amani na Maendeleo wa China na Umoja wa Mataifa, na imeenezwa katika nchi zaidi ya 100.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma