Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

VI. Mkutano wa Kwanza wa Amani, Utawala Bora na Maendeleo kati ya China na Pembe ya Afrika wafanyika kwa mafanikio

Mkutano wa Kwanza wa Amani, Utawala Bora na Maendeleo Kati ya China na Pembe ya Afrika ulifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia Tarehe 20 hadi 21, Juni, 2022. Mjumbe Maalumu wa Masuala ya Pembe ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Xue Bing (katikati), mawaziri na wawakilishi wa ngazi ya juu wa nchi za Pembe ya Afrika ambazo ni Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Uganda na Djibouti walihudhuria kwenye mkutano huo.

Pendekezo la "Mtazamo wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika" lilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi wakati alipofanya ziara nchini Kenya mapema Januari mwaka huu, ili kuziunga mkono nchi za eneo hilo katika kushughulikia changamoto za usalama, maendeleo na utawala bora.

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha