

Lugha Nyingine
Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022
III. Malawi na China zatia saini makubaliano kuhusu ushirikiano wa BRI
Malawi na China zilitia saini mkataba wa maelewano (MOU) kuhusu ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) Tarehe 23, Februari mjini Lilongwe, ambapo Malawi imekuwa nchi ya 149 kujiunga na mradi huo wa kimataifa.
Katika hafla ya utiaji saini, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Nancy Tembo ameeleza kuwa kujiunga na BRI kutatoa msukumo mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Balozi wa China nchini Malawi Liu Hongyang amesema China iko tayari kuunganisha BRI na Dira ya 2063 ya Malawi, na kuchangia jitihada za Malawi katika kujenga taifa lenye utajiri shirikishi na linalojitegemea.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma