Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

VIII. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan afanya ziara nchini China

Kutokana na mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Tarehe 2 hadi 4 , Novemba. Katika ziara yake, Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hapa Beijing. Marais hao wawili wametangaza kuinua uhusiano baina ya nchi hizo mbili hadi kufikia ngazi ya wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote.

Rais Samia alikuwa mkuu wa kwanza wa nchi ya Afrika ambaye China imepokea baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). 

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha