Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

IV. Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere chazinduliwa

Tarehe 23, Februari, Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilizinduliwa nchini Tanzania, ambapo Rais wa China Xi Jinping alituma barua ya pongezi kwa uzinduzi wake, na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwaongoza mamia ya wananchi na viongozi wawakilishi wa nchi sita za Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika uzinduzi wa shule hiyo.

Chuo hicho kilianzishwa kwa pamoja na vyama sita vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika: Chama Cha Mapinduzi cha Tanzania (CCM), Chama cha African National Congress cha Afrika Kusini (ANC), Chama cha Ukombozi cha Msumbiji (FRELIMO), Chama cha Harakati ya Ukombozi wa Watu cha Angola (MPLA), Chama cha SWAPO cha Namibia na Chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe.

Ujenzi wa chuo hicho umefadhiliwa na Serikali ya China chini ya ushirikiano wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama hivyo vya ukomboni vya Kusini mwa Afrika na umegharimu takribani dola za kimarekani milioni 45. Mwaka 2018 aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo. 

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha