

Lugha Nyingine
Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (9)
IX. Bidhaa za Afrika zaonekana kwenye Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE)
Katika mwezi wa Novemba, kwenye eneo la chakula na mazao ya kilimo la Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), kahawa ya Ethiopia, mivinyo ya Afrika Kusini na maparachichi ya Kenya na bidhaa nyingine kadha wa kadha kutoka Bara la Afrika zinaonekana kwenye rafu, zikileta “ladha ya Afrika” inayowavutia Wachina.
Tangu China ilipotangaza kuanzisha utaratibu wa mazao ya kilimo kutoka Afrika kupita forodha za China kwa urahisisi mwezi wa Novemba mwaka jana, bidhaa nyingi zaidi za kilimo kutoka bara hilo zimeingia China. Katika mwezi wa Agosti mwaka huu, shehena ya kwanza ya parachichi kutoka Kenya imeingia katika soko la China. Licha ya hayo, machungwa kutoka Afrika Kusini, na ufuta kutoka Tanzania pia umeingia soko la China kwa kupitia utaratibu uliorahisishwa.
Takwimu kutoka Idara ya Forodha ya Shanghai zinaonesha, katika miezi minane ya kwanza ya Mwaka 2022, forodha hiyo imepitisha mazao ya kilimo yenye thamani ya Yuan bilioni 47.2 kutoka Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma