

Lugha Nyingine
Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022 (7)
VII. Wanaanga wa China wazungumza wakiwa anga ya juu na vijana wa nchi mbalimbali za Afrika
Tarehe 6, Septemba, Wanaanga watatu wa China walizungumza wakiwa kwenye anga ya juu na vijana kutoka nchi nane za Afrika kwa njia ya video, wakibadilishana uzoefu wao katika misheni ya Chombo cha anga ya juu cha China cha Shenzhou-14.
Ukumbi mkuu wa shughuli hiyo iliyopewa jina la "Ongea na Wanaanga," ulikuwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia huku wanafunzi kutoka Algeria, Misri, Ethiopia, Namibia, Nigeria, Senegal, Somalia na Afrika Kusini wakishiriki katika mhadhara huo kwenye kumbi ndogo. Wawakilishi vijana kutoka nchi hizo wameuliza maswali yanayohusu masuala kadhaa yakiwemo namna Jangwa la Sahara na Mlima Kilimanjaro unavyonekana kutoka anga ya juu n.k.
China siku zote inatilia maanani sana kutekeleza ushirikiano na nchi za Afrika katika sekta ya usafiri kwenye anga ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma