Matukio muhimu ya kipekee ya mawasiliano na mabadilishano kati ya China na Afrika Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

China na nchi za Afrika zimeendeleza urafiki wao wa jadi Mwaka 2022, zikitekeleza ushirikiano wa kivitendo kwenye sekta za siasa, biashara, uchumi na diplomasia na kupata matunda kemkem. Katika wakati huu ambapo mwaka mpya unawadia, toleo la Kiswahili la tovuti ya Gazeti la Umma (People’s Daily Online) limeteua na kujumuisha matukio kumi muhimu ya kipekee ya mawasiliano kati ya China na nchi za Afrika. Hebu tusome pamoja ushirikiano wa siku zilizopita, tukitarajia matunda mengi zaidi kati ya pande hizo mbili yatapatikana katika siku za baadaye.

I. Waziri wa Mambo ya Nje wa China atembelea Eritrea, Kenya na Visiwa vya Comoro wakati wa mwaka mpya

Kuanzia Tarehe 4 hadi 7 mwezi wa Januari, 2022, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amealikwa kutembelea Eritrea, Kenya na Visiwa vya Comoro. Kutembelea nchi za Afrika kwanza mwanzoni mwa kila mwaka ni utamaduni wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China. Wang Yi alisema, ingawa kuna changamoto ya maambukizi ya virusi mwaka huu, China imewasili Bara la Afrika kama ahadi yake ilivyosema.

Katika ziara hiyo ya Bw. Wang, China na Eritrea zimekubaliana kujenga uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili; China na Kenya zimetia saini mikataba sita kuhusu ushirikiano kwenye sekta ya uchumi wa kidijitali, uwekezaji, uuzaji mazao ya kilimo na uvuvi kwa China na kadhalika; na pia Waziri Wang alizungumzana na Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani, wakisisitiza tena msimamo wa kuungana mkono katika upande wa mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa pande zote.

 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha